Job alertsNovember 2, 2022

Tangazo la Kazi: Mhariri Msaidizi

Cheo: Mhariri Msaidizi (Mkataba wa kazi maalum)

Eneo: Dar es Salaam, Tanzania

Mkataba: Miezi 6 (utaongezwa kulingana na utendaji)

 

Kuhusu Jamii Media

Kampuni ya Jamii Media ni kampuni iliyosajiliwa nchini Tanzania. Jamii Media hufanya kazi na vyombo vya habari, asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa na taasisi mbalimbali kuandaa na kutekeleza miradi yenye tija kwa taasisi hizo na umma wa watanzania. Kampuni inafanya miradi mbalimbali kama vile uzalishaji wa maudhui ya redio na mitandao ya kijamii, mafunzo kwa vyombo vya habari na asasi za kiraia. Pia kampuni husaidia mashirika haya katika matumizi bora ya teknolojia, biashara na mitandao ya kijamii katika kutimiza malengo yao. Tembelea tovuti yetu kujua zaid.

 

Muhtasari wa nafasi ya kazi

Jamii Media inatafuta Mhariri Msaidizi anayeweza kufanya utafiti, kuandika, kuhakiki uandishi, na kuchapisha maudhui ya mtandaoni. Nafasi hii iko wazi kwa mwandishi mwenye ujuzi wa kidijitali na jicho la uhariri. Mhariri msaidizi atakuwa na jukumu la kusimamia na kuhariri tovuti ya habari ya masuala yanayojiri na pia kuhariri na kuwashauri wanufaika wa mradi wetu (Vyombo vya habari vya mtandaoni 20). Mhariri msaidizi atamsaidia Mhariri Mkuu kupitia mawazo ya awali ya maudhui (Story pitch) na kushauri maudhui yapi yatengenezwe, ambayo yatavutia wasomaji/watamaji wengi. Katika jukumu la kupitia mawazo hayo, utatoa mawazo ya kurekebisha maudhui hayo na kushauri vichwa vya habari vinavyotakiwa kutumika.

 

Majukumu muhimu:

Chagua mada ya wiki ya kutengenezwa na wanufaika, iliyo ya kimkakati na yenye maslahi kwa jamii.

 • Kuwasiliana na wanufaika, hakikisha tarehe za uchapishaji wa maudhui tulizokubaliana zinafuatwa, kusimamia na kufuatilia uwasilishaji wa maudhui kutoka kwa washiriki.
 • Kuangalia ubora wa maudhui yaliyotengenezwa na kuhakikisha kwamba mwongozo wa muundo wa maudhui unafuatwa na wanufaika.
 • Kufanya kazi kwa ukaribu na afisa ufuatiliaji na tathmini katika kufanya uchambuzi wa maudhui ya vituo vya habari na mchango wake kwa jamii.
 • Kutoa mrejesho kwa wanufaika, kama vile kujibu maswali na kutoa ushauri wa kitaalamu pale unapotakiwa.
 • Kufanya kazi kwa karibu na afisa mkuu wa mradi na mhariri mkuu kutengeneza tovuti (blog) ya habari ya masuala yanayojiri.

 

 Uzoefu na ujuzi unaohitajika:

 

 • Ujuzi wa kisekta: Uandishi wa habari, uandishi wa nakala, Uhadithiaji, Uhariri, Usimamizi wa maudhui, uelewa wa mitandao ya kijamii.
 • Ujuzi wa kiufundi: Microsoft Office Suite, Google Forms, Google Docs, Google Presentation
 • Ujuzi wa kiujumla: Mawasiliano, Ubunifu, Umakini hata kwa vitu vidogo, Kusimamia muda, Utafiti
 • Ujuzi mkubwa wa kuwasiliana kwa kuongea na kuandika kwa ubunifu kuandika kwa lugha zote, Kiswahili na Kiingereza
 • Uzoefu katika mawasiliano, hasa mawasiliano ya tafiti au uandishi wa habari wa data, usimamizi wa mradi, ufuatiliaji na tathmini, usimamizi wa maarifa, uandishi wa habari, vyombo vya habari vya kidijitali na maendeleo.
 • Shahada ya kwanza katika uandishi wa habari ni nzuri, ila tunazingatia zaidi uwezo wako wa kukamilisha kazi vizuri.

 

TUMA MAOMBI HAPA kabla ya November 8, 2022

 

 

Share